0
Zanzibar                                                              02 Novemba, 2023

 Mdahalo wa wadau sheria na utawala bora Zanzibar wamekutana katika kikao kazi cha kujadili na kupeana mbinu zitakazoweza kuwawezesha kutatua matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii hasa katika nyanja ya sheria.

Katika kikao kazi hicho cha majumuisho kilichohudhuliwa na wadau kutoka taasisi binafsi na serikali likiwepo jeshi la polisi nchini, Mwenyekiti wa taasisi ya ZAFAYCO iliyoendesha mdahalo huo ndugu Abdalla Abeid amesema, wadau wote wanapaswa kujua njia raisi zitakazoweza kuwafanya wananchi kujifunza na kuona wepesi wa sheria. 

 Pia katika kikao jumuishi ya majadiliano ya kikao kazi hicho wadau wameweza kutoa majumuishi ili kuweka kuisaidia jamii hasa katika hatua itakayoweza kuwapa nafasi kuona sheria ni msaada na kimbilio wakati wote.

Pamoja na hayo imependekezwa upatikanaji wa madodoso ya sheria huko mtaani kupatikana kwa urahisi ili kuwafanya wananchi kujifunza kwa kusoma kwa urahisi kwa lugha rahisi ile inayoeleweka kwa wananchi walio wengi.



    HABARI KATIKA PICHA
👆Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya ZAFAYCO Abdalla Abeid akiongea wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa wadau kuhusu jukumu la kuzingatia utawala wa sheria Zanzibar.


👆 Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa ZAFAYCO ndugu Abdalla Abeid (picha ya chini) wakati wa kufungua Mdahalo huo.




👆 Mkuu wa Kitengo cha Mipango Taasisi ya ZAFAYCO Bi. Aziza Jaffar Ismail akiwasilisha kwa wadau moja ya mada iliyochagiza wakati wa mdahalo wa mapema.



👆 Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakisikiliza uwasilishaji wa mada wakati wa majadiliano ya moja kwa moja, wakati wa kufungua Mdahalo huo.


👆 Picha ya pamoja kwa wadau wa Taasisi mbalimbali waliohudhulia mdahalo na majadiliano iliyoangazia upande wa jukumu la kuzingatia utawala wa sheria Zanzibar.


Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top