0
DAR ES SALAAM
Asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu kwa Tanzania kupata katiba mpya na asilimia 56 wanasema toleo la mwisho la rasimu ya katiba lipigiwe kura na wananchi. Hata hivyo, asilimia 48 ya wananchi wanasema kwa maoni yao, katiba mpya haitapatikana ndani ya miaka mitatu ijayo.


Habari kwa ufupi

Hata hivyo, wananchi wamegawanyika kwenye baadhi ya hatua za uwajibikaji zilizopendekezwa ikiwemo kuzuia viongozi na watumishi wa umma kuwa na akaunti nje ya nchi (asilimia 52 wanaunga mkono), kuwepo kwa ukomo wa ubunge (asilimia 52 wanaunga mkono) na kuweka kanuni za uwazi na uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu za taifa (asilimia 48 wanaunga mkono).

Hivi vyote ni vipengele vya rasimu ya katiba ambavyo viliondolewa na Bunge Maalumu la Katiba. Pia, wananchi wanaunga mkono kuondolewa kwa kipengele kinachotaka kuchunguza na kudhibiti ofisi ya Rais (asilimia 55) pamoja na mawaziri kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge (asilimia 62). 


Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Zege imelala? Maoni ya wananchi kuhusu kukwama kwa mchakato wa kuunda katiba mpyaMuhtasari huu unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,745 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye utafiti huu) mwezi Juni hadi Julai 2017. 


Profile PHOTO: Mkurugenzi mkuubwa Twaweza nchini Aidan Eyakuze. 
“utafiti huu umedhihirisha uwajibikaji wa siasa kwenye uhalali wa mchakato wa katiba. Matokeo yameonesha dhahiri kwamba wananchi wengi wanatatizwa katika kutofautisha kitendo cha UKAWA kugomea bunge la Katiba na migomo mingineyo. Ushabiki wa kisiasa huwafanya watu wengi kutozingatia uhalali wa jambo husika. Hivyo basi; vyovyote tutakavyofufua mchakato wa katiba, ni muhimu sana kwa wahusika wakuu kuheshimu na kutambua kwamba sheria mama ya nchi ni ya thamani zaidi kuliko tofauti za kisiasa. Tanzania inahitaji mchakato wa katiba utakaozingatia uhalali na ujumuishi wa watanzania wote” Alisema Aidan Eyakuze

Post a Comment

 
Top