Mkuu wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia wanachuo wote waliomaliza
masomo yao katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Kampasi zote za (Dar es
Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga na Mbeya) kwa muhula wa Septemba 2017
hadi January 2018 kuwa mahafali yao yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Mei
2018 katika kampasi ya Chuo cha Utumishi wa Umma jijini Mbeya.
Chuo kipo mkabala na
Soko matola umbali wa takriba kilomita 3 kutoka Stendi kuu ya Mabasi na Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.
Kila mhitimu anatakiwa
kuzingatia yafuatayo:- Kuthibitisha ushiriki kabla ya Siku ya Jumatano tarehe
23 Mei 2018 kwa barua au simu ya Ofisi ya usajili kampasi ya Mbeya Simu:
0252502627 Simu za Mkononi: 0719393962, 0755034213, 0682774700, 0717568787,
Whatsapp only: 0789056331, Email: mbeya@tpsc.go.tz
Gharama za kukodi skafu
ni Shs. 10,000/= (Hairudishwi) Malipo ya skafu yafanyike kupitia Jina la
Akaunti: Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Mbeya, Namba ya Akaunti: 0150019909102
CRDB BANK MBEYA BRANCH)
Zoezi la mwisho (Rehearsal)
itafanyika siku ya Alhamisi tarehe 24
Mei 2018 saa 8:00 mchana kwenye eneo yatapofanyika Mahafali. Majina ya wahitimu
tembelea wavuti ya chuo: www.tpsc.go.tz kabla ya Jumatano tarehe 02 Mei 2018.
Wahitimu wote
wanatakiwa kuvaa suti rangi nyeusi au “darkblue” na mashati meupe.
Post a Comment