0
   📍 ZANZIBAR

 Sera iliyoanzishwa na inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi iliyoanzishwa mwaka 2014, inahakisi katika kuwapa uwezo wananchi walio katika hali ya chini na kuweza kukuza vipato na uwezo wa kimaisha. 

Akifungua mkutano huo wa mwaka wa mapitio ya ulinzi wa jamii, Waziri wa Maendelo ya Jamii, Jinsia Wazee  na Watoto Zanzibar, Mheshimiwa Riziki Pembe Juma amesema Serikali ina mpango wa kuwafikia wananchi wote ambao ni masikini na hasa wazee ili kuwaondoa katika hali duni ya kimaisha na kuwawezesha kiuchumi.

Vilevile katika tathimini ya kutambua wazee waliopo maeneo mbalimbali Zanzibar, imefahamika wazee 24,776 waliandikishwa kwa visiwa vyote vya Unguja na Pemba, kupitia tathimini hiyo ambapo serikali ilikuwa ikimlipa kila mzee kila mwezi kiasi cha shs 20,000/- .

Hata hivyo Serikali ya mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Daktari Hussein Mwinyi iliweza kuongeza malipo ya kila mwezi kwa wazee kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 50,000 ambayo wazee hao wanapokea kwa mwaka huu.

Katika hatua nyingine serikali imeweza kuiwezesha familia inayopata watoto watatu wanaozaliwa kwa maramoja kiasi cha shs 30,000 ili iweze kuwawezesha kuwapa uwezo kujikimu kwa kipindi cha ulezi watoto hao.



  HABARI KATIKA PICHA.
        PICHA: Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia Watoto –UNICEF, Bi Laxmi Bhawani, akiongea wakati wa kufungua mkutano huo wa mwaka mapema leo mjini Zanzibar.



        PICHA: Baadhi ya waandaaji wa Mkutano huo (kutoka kulia) Miss. Hafidhuu Said Salum Afisa Habari na Mawasilinao wa Wizara (katikati) Mr. Lahdad Haji Chum ambaye ni Mkuu wa divisheni ya Ustawi wa Jamii. 



        PICHA: Katibu mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Abeda Rashid Abdullah akiongea kabla ya kumkaribisha Waziri ambapo ambapo amezishauri taasisi zote kuweza kutumia mkutano huo kuendeleza yote watakayojifunza.


       PICHA: Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar Mheshimiwa Riziki Pembe Juma akiongea katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka.



        PICHA: Baadhi ya wshiriki wa mkutano huo wakifuatilia na kusikiliza hotuba kutoka kwa waziri (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.





Photo's Copyright Leonard Mutani.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top