0

📍 Zanzibar.

Kongamano la kimataifa la usimamizi wa biashara na maendeleo ya uchumi, limefunguliwa mjini Zanzibar na makamu wa pili wa Rais Mh. Hemed Suleiman, alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Mh, Dr. Hussein Ali Mwinyi.


PICHANI: Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano.


PICHANI: Watalaamu na Watafiti wakimsikiliza Mgeni rasmi akiongea (picha ya juu) wakati wa ufunguzi wa Kongamano.



PICHANI: Waziri katika Ofisi ya Rais Fedha Mh. Saada Mkuya akiongea wakati ufunguzi na kuchangia kwa ujumuishi wa mada ya kwanza iliyowasilishwa katika kongamano hilo.





PICHA: Viongozi wa Dini kushoto na baadhi ya wadau wa Kongamano wakisikiliza kwa makini. 


PICHANI: Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar (kushoto) akimpatia cheti cha kutambua kufika na kutoa mada katika kongamano hilo kwa ndugu Gleb Sugakov kutoka nchini Urusi.


HABARI KWA UNDANI.

Ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa hatua ya kuleta kongamano hili Zanzibar ni kuleta umoja kwa wachumi, wasomi kutoka pande zote kwa pamoja katika misingi ya utafiki ambapo majadiliana yatakayofikiwa yataleta hatua ya kuweza kutatua changamoto zinazilikabili taifa.

Pia ameendelea kusema kuwa nchi yetu imeweka dira na misingi yenye kuleta uchumi imara ambao utakuwa na faida kwa wananchi wote kwa pamoja, huku serikali ikijua sekta binafsi ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchuni wa nchi yetu.

Ameendelea kusema kuwa "Tafiti za nje hazina faida kwa nchi zetu kwa sababu hazina uwiano na mazingura ya nchi zetu" hii ni kutokana wanaofanya tafiti wakiwa nchi mwao ambapo mazingira yao hayana ufanano wa kisayansi na hapa kwetu, hivyo watafiti wa hapa nyumbani wana nafasi kutumia mlango huo kuweza kutoka na kuweka wazi tafiti zao kwa jamii.

Kongamano kama hili likitumika vizuri litaleta mbinu nzuri na ubunifu mpya kwa wataalam wetu badala ya kutumia na kutegemea bunifu  kutoka nje ya mataifa yetu ya afrika. 

Kongamano hilo lililowashirikisha wasomi kutoka nchi zaidi ya 6 zikiwepo Urusi, Ghana, Rwanda, Kenya na mwenyeji Tanzania, unaangazia kuangazia majadiliano ya kitaaluma kutoka kwa watoaji mada mbalimbali.

Naye Waziri wa nchi ofisi ya Rais fedha Zanzibar mheshimiwa Saada mkuya amesema katika tafiti mbalimbali nchi nyingi hivi sasa zimejikita kuwapa uwezo wananchi wao ili kukuza ujuzi.

Ametoa mfano wa nchi kama Singapore ambayo imetumia watafiti na wasomi mbalimbali wa nchini mwao ili kufikia malengo hatirifu, pamoja na kongamano hili kufanyika hapa Zanzibar iwe ni hatua kubwa katika nchi yetu.

"Taasisi hii inekuja Zanzibar ikiwa na sisi wazanzibari tayari tuna taasisi yetu ijulikamayo kama ZIYAT ilianza kazi ikiwa na lengo la kusimamia wadau wa fedha" alisema Mh. Saada Mkuya.



Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top