0
Profile PHOTO: Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Katika hatua inayoleta utata, shirika la afya duniani-WHO limemteuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kuwa balozi wa hisani barani Afrika ili kusaidia kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kama vile mshtuko wa moyo, kiharusi na pumu.
Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus mwafrika wa kwanza kuongoza idara hiyo ya Umoja wa Mataifa amekosolewa vikali na wapiga kampeni wa kimataifa wa haki za binadamu pamoja na wanaharakati wengine kwa kufanya uteuzi huo.
Wakati huo huo mkurugenzi mtendaji wa U.N Watch, Hillel Neuer alisema katika taarifa yake kwamba serikali ya Robert Mugabe inawakandamiza wanaharakati wa haki za binadamu, inapinga demokrasia na kuligeuza taifa hilo na mfumo wake wa afya kuingia katika hali mbaya ya kiuchumi.

Source: VOA

Post a Comment

 
Top