0

 πŸ“Zanzibar.

Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mh. Hemed Seleiman amefungua Kongamano la tano (5) la watoa huduma ya dawa za dharura mapema leo katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport liyopo Kiembesamaki Zanzibar.

Katika hotuba yake aliyomuwakilisha Rais wa Zanzibar Mh. Dkt. Husemsein Mwinyi, amewataka watoa huduma za dharula nchini kuangalia na kuboresha utoaji wa huduma zao.

Katika kongamano hilo lililojikita kuendeleza mifumo ya huduma ya dharura na dhabiti kwa ajili ya chanjo endelevu ya afya kwa wote nchini Tanzania imewakutanisha wadau wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa pande zote mbili Tanzania bara na Visiwani. 

Pamoja na hayo, waziri wa Afya Zanzibar Mh. Hassan Mazrui ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kuongeza uwezo kwa watoa huduma ili kuendana na mazingira wanayokumbana nayo wawapo kwenye utendaji.

Hata hivyo ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance kwa kila mkoa hapa nchini. 


 HABARI ZAIDI KATIKA PICHA.

PICHA ☝🏽: Mheshimiwa Hemed Seleiman (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa Taasisi ya EMAT Chiku Juma (kulia) jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi zake.



PICHA ☝🏽: Daktari Saidi Kilindimo (kulia) wa idara ya magonjwa ya dharula chuo kikuu cha Muhimbili akimpa maelezo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Seleiman (kushoto) maelezo jinsi ya kufanya utafiki wa mwili wa mgonjwa pasipo kupasuliwa, kutokana na teknolojia waliyo nayo.


PICHA ☝🏽: Daktari Juma Mfinanga ambaye ni bingwa wa magonjwa ya dharula wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiongea wakati wa kufungua kongamano hilo mapema leo mjini Zanzibar.

PICHA ☝🏽: Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassoro Mazrui akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano ambapo ameipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuboresha huduma za afya na baadaye alimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano hilo.


PICHA ☝🏽: Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Hemed Seleiman akiongea na wadau wa sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano.

PICHA ☝🏽: Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais Mh.Hemed Seleiman (katikati) mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Mh. Kitwana (kushoto) Waziri wa afya Zanzibar Nassoro Mazrui (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya ufunguzi wa kongamano

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top