π ARUSHA.
Taasisi ya Sayansi ya Teknolojia Afrika ya Nelson Mandela imempokea mkuu mpya wa Taasisi hiyo baada ya aliyekuwa mkuu wa Taasisi hiyo Mh. Mohamed Gharib Bilal Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumaliza muda wake.
Katika hafala ya makibidhiano iliyofanyika chuoni hapo jijini Arusha makamu mkuu wa Taasisi mstaafu Dkt. Mohamed Bilal amekishukuru Chuo hicho kwa muda wote wa utumishi wake, akiwa ndiye Mkuu wa Taasisi wa kwanza tangu kuanzishwa kwake.
Pamoja na hilo amemuomba Mkuu mpya wa chuo Mh. Omari Issa kuwa kuendeleza yale yote mazuri ili kuweza kukipaiwha chuo hicho.
Aitha Mkuu Mpya wa Chuo Mheshimiwa Omari Issa amemshukuru aliyekuwa mkuu wa Taasisi hiyo Dr. Mohamed Bilal kwa muda wote wa uongozi wake kwa kukiwezesha Chuo kufikia hatua kubwa na kuifanya Taasisi ya Nelson Mandela kuwa moja ya Taasisi kubwa barani Afrika.
Habari zaidi katika picha.  |
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.