0

Zanzibar.                                                                   

Mkutano wa wadau wa sekta ya Afya wenye lengo la kutokomeza ugonjwa wa Maralia katika mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar umefunguliwa na mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi ukiwa na lengo la kuhakikisha ugonjw huo unatokomezwa.

Katika mkutano huo uliohudhuliwa  na wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa usafirishaji-Bodaboda, Mama Lishe, wadau wa Utalii na Wananchi, umeangazia maeneo ya mji mkongwe ambapo ni eneo au jicho la uchumi wa mkoa huo.

Akifungua mkutano huo wa siku moja, Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Mh. Idrissa Kitwana amesema kuwa, ugonjwa huu wa Maralia unaweza kumalizika endapo wananchi watashirikishwa moja kwa moja maana wanaosababisha ugonjwa huo ni wafanyabiashara na watu mbalimbali kutokana na eneo hilo kuwa na muingiliano  mkubwa  kwa wageni na watu mbalimbali.

Vilevile ameendelea kusema mkoa wa mjini Magharibu ni kioo nani eneo ambalo ni sawa na ‘Mecca’ kwamba kila mtu lazima afike, hivyo hakuna jinsi lazima njia za msingi zichukuliwe ili kuweza kupunguza maambukizi ya ugonwa huo.

Pia ametoa wito kwa wananchi kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa, kuzuia umwagajiwa ovyo wa maji, kumwaga ovyo uchafu na kila mtu awe na utaratibu wa kwenda kupima afya.

Tusipake rangi kuhusu malaria kuwa ni Mbu tu, bali uchafu ni chanzo kikubwa cha mbu wa maralia

Pamoja na hayo Programu Meneja wa mradi wa tokomeza Malaria Zanzibar Shija Joseph Shija anasema mpango mkakati wa kutokomeza malaria ambapo kesi za marali kwa mwaka huu kimeshuka kufikia chini ya asilimia, pia uchunguzi unaonyesha kuwa mgonjwa wa maralia hajiamini akiambiwa hana maralia, hivyo upelekea kwenda kituo kingine cha afya kucheki afya kwa mara ya pili.


    👆PICHA Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr. Salim Slim, akiongea wakati wa utoaji wa taarifa za Afya na Maralia, kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi.


    👆PICHA Wadau wakifuatilia mkutano uliohainisha elimu na jinsi ya kutokomeza Maralia mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.



     👆PICHA Programu Meneja wa mradi wa tokomeza Malaria Zanzibar Shija Joseph Shija  {kulia} akiongea wakati wa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya hali ya ugonjwa wa Maralia Zanzibar.


     👆PICHA: Baadhi ya viongozi na Wananchi kutoka maeneo tofauti ya Mkoa wa Mjini Magharibi wakifuatilia na kusikiliza hotuba, katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar.



    👆PICHA: Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mh. Idrissa K. Mustafa, akiomngea wakati wa kufungua mkutano wa kujadili hali ya Maralia katika eneo lake, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Golden Tulip Airport - Kiembesamaki Zanzibar.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top