0

📍ZANZIBAR.

Maonyesho ya sikukuu ya Wakulima nane nane Zanzibar yamehitimishwa ambapo Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Zanzibar Mh. Shamata Shaame Khamis, amesema kuwa maonyesho ya mwaka huu yamekuwa na hamasa kubwa. 

Waziri wa nchi ofisi, ofisi ya Waziri mkuu (sera, bunge na uratibu) Mh. Jenista Mhagama amesema, maonyesho haya yana viwango kutokana na aina waonyeshaji wake kujipanga na kuonyesha aina mbalimbali za ubunifu na utunzaji wa mazingira pamoja na mazao.

Aliendelea kusema kwa kuwataka wakulima kutumia maonyesho hayo kujifunza mbinu bora za uzalishaji pamoja kutumia pembejeo za kisasa ili kuvuna mazao mengi na yenye ubora.











👈PICHA:
Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Zanzibar, Mh. Shamata Shaame Khamis akiongea wakati wa kufunga sherehe za nane nane Dole Kizimbani Zanzibar.








👈PICHA:
Mh. Jenista Mhagama ambaye ni Waziri wa nchi ofisi, ofisi ya Waziri mkuu, akihutubia wanaanchi (hawapo pichani) wakati wa ufungaji wa maonyesho ya nane nane Dole Kizimbani Zanzibar.











👈 PICHA:
(Kulia) Ismail Mohamed Hamed kutoka kampuni ya BIZAGROVET akipokea Tuzo ya kutambuliwa kama mfugaji na mzalishaji bora kutoka kwa Mh. Waziri Jenista Mhagama.


👈 PICHA:
Mh. Waziri Jenista Mhagama akimnywesha maziwa mwanafunzi (jina alikuweza kupatikana) wakati wa kuhitimisha unywaji wa maziwa katika maonyesho hayo ya nane nane Dole Kizimabani Zanzibar.
-Kulia kwa waziri ni Katibu mkuu Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji Seif Shaaban Mwinyi na mwenye kofia ni Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Zanzibar Mh.Shamata S. Hamis.









👈 PICHA:
Mh. Waziri Jenista Mhagama akinywa maziwa na wanafunzi waliohudhulia uhitimishaji wa maonyesho kwa unywaji wa maziwa katika maonyesho hayo ya nane nane Dole Kizimabani Zanzibar.
-Kulia kwa Mh. Jenista, mwenye kofia ni Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Zanzibar Mh.Shamata S.Hamis.


Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top