Zanzibar.
Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaib Hassan Kaduara amefunga Kongamano la Maji lililofanyika mjini Zanzibar kwa siku mbili, kongamano hilo liliudhuliwa na takribani watu 250 kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo katika ufunguzi wake Mhe. Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nduye alikuwa mgeni rasmi.
Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Kaduara alitoa shukurani kwa Wizara ya Maji ya Serikali ya Muungano wa Tanzania iliyowakilishwa na Bi Meri Prisca Mahundi ambaye ni Naibu Waziri wa Maji kwa ushirikiano uliochochea mabadiliko katika sekta ya maji Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambapo wananchi wa pande zote mbili wanaendelea kufurahia huduma ya maji safi na salama.
Aidha amepongeza majadilianpo yaliyofanyika kwa siku zote mbili sababu umeleta tija visiwani Zanzibar na kusema kuwa ni jambo la kujivunia na muhimu sana kwa nchi yetu kwani litatoa fursa kwa washiriki wa ndani na nje ya nchi kuwa na umoja, kujenga mtandao utakaowezesha kubadilishana mawazo na uzoefu na kuleta ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa masuala ya maji.
Pamoja na hayo amewaomba wadau mbalimbali na washirika wa maendeleo kuendelea kushirikiana na watafiti tafiti zao, ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kunufaika na upatikanaji wa huduma bora za maji safi na salama na kufikia heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu hassan kuhusu kumwangusha ndoo kichwani mama huyo.
👆PICHA: Naibu Waziri wa Maji kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mh. Meri Prisca Mahundi, akiongea wakati wa kufunga kongamano la Maji katika Hoteli ya Verde Zanzibar. |
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.