📍ZANZIBAR.
Spika wa Baraza la Wawakilishi (BLW) Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid ametembelea maonyesho ya wakulima nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Dole Kizimbani mjini Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda kadhaa na kujionea maendeleo mbalimbali ya kilimo na uzalishaji mbalimbali amesema, nimeona uzalishaji wa Samaki wa maji baridi kama Sato kuanza kuzalishwa katika maji chumvi, hii ni hatua kubwa katika visiwa vyetu vya Zanzibar.
Vilevile amewaomba wananchi kutembelea maonyesho hayo kuweza kujionea miche mbalimbali kama Mwembe ambao unaweza kutoa matunda manne ya aina tofauti katika mche mmoja.
👆PHOTO:
Spika wa Balaza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid (kulia) akiangalia vipeperushi na kupata maelezo kutoka kwa Meneja mauzo wa NMB kanda ya Zanzibar Muhsin Nahodha (kushoto) alipotembea banda hilo lilipo katika maonyesho hayo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.