Mamlaka inayosimamia bonde la mto pangani, imewakutanisha wadau mbalimbali katika kikao kazi cha kuweza kuweka usimamizi na matumizi sahihi ya upatikanaji, matumizi na ulinzi katika vyanzo mbalimbali vya maji.
Katika kikao hicho cha siku moja kichowakutanisha watendaji wa mitaa, kata na wilaya za jiji la arusha kiliangazia changamoto mbalimbali za upatikanaji wa rasilimali maji ikiwa ni katika kupatikana kwa njia itakayoweza kutatua na kupata njia bora ya kutunza vyanzo.
Aidha mamlaka hiyo iliyopewa jukumu la kulinda vyanzo vyote vya maji inawajibu kisheria kusimamia rasilimali maji ili itumike kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Vilevile wadau hao wamefikia maamuzi kwa watendaji wote kuwa mstari wa mbele kusimamia na kutia elimu nwa wananchi wanaoishi na wanaotumia maji ili kutunza rasilimali hiyo.
PICHA:☝️Kwa niaba mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa arusha Richard kwitega ambaye aliwakilishwa na msaidizi wake (pichani) akiongea na wadau mbalimbili katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa mapema leo.
PICHA: ☝️Wadau walioshiriki katika kikao cha siku moja kichowakutanisha watendaji wa mitaa, kata na wilaya za jiji la arusha wakimsikiliza mwakilishi wa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufungua kikao hicho.
PICHA:☝️Mkurugenzi wa mamlaka ya bonde la mto pangani Segule segule (kulia) akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao hicho pembeni yake ni mwakilishi wa mgeni rasmi katibu tawala mkoa wa arusha Richard kwitega.
PICHA:☝️Picha ya pamoja ya viongozi waandamizi wa mamlaka ya bonde la pangani na akiwepo mkurugenzi wa bonde la mto pangani (mwenye suti ya blue) na mwakilishi wa katibu tawala Arusha (wa tatu kulia) wakati wa kikao kazi hicho.
Post a Comment