ARUSHA.
Tanzania imekuwa ikipokea na kuhifadhi wakimbizi kwa miongo zaidi ya sita ikiwa ni kabla na baada ya kupata uhuru hii inatokana na nchi nyingi zinazoizunguka kuwa na vita vya wenyewe hama migogoro inayozalisha wakimbizi.
Hayo yameelezwa na Waziri wa mambo ya ndani George Simbachawene katika mkutano wa maandalizi ya uandishi wa kitabu kuhusu miaka 60 ya kuhifadhi wakimbizi nchini unaofanyika jijini Arusha, "kuwa kipindi chw pili cha kuhifadhi wakimbizi kilianza miaka ya 1990 hadi sasa na kuendelea, waziri ametoa rai kwa jumuhiya ga kimataifa kuzisadia nchi zenye wakimbizi ikiwemo Burundi" Alisema.
Vilevile Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Diginity Kwanza ya Tanzania, ametanabaisha ushiriki wa Tanzania kuwa ni nchi pekee katika ukanda wa maziwa makuu ambayo imekuwa na amani siku zote, hali inayopelekea kuamini kuwa hizo ni baraka na wengine, miongoni mwa neema nyingi, mkurugenzi wa shirika la Diginity Kwanza Janemarry.
"Serikali ya Tanzania imekuwa serikali inayojali haki, utu pamoja na haki za kibinadamu, kuzuia unyanyasaji kwa wakimbizi, watu wenye matatizo ya kisiasa wanaotafuta hifadhi kwenye mazingira ya usalama" Amesema.
Naye Mkurugenzi mkaazi wa shirika la wakimbizi nchini Antonia Jose Canhandula amesema kuwa, pamoja na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayofanya wananchi wake kujivunia amani, ambayo inatunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo kupitia uandishi wa kitabu kinachotarajowa luzinduliwa muda mfupi ujao.
"Tanzania bado inaendelea kuwa kati ya nchi chache barani Afrika kuruhusu aridhi yake kutumiwa na wananchi wa taifa lingine, kupitia kitabu hicho itakuwa ni sehemu mojawapo ya kuwapa elimu kizazi kijacho ili kujivubia tunu hii."
PICHA: Waziri wa katiba na sheria, George Simbachawene akiongea wakati wa kufungua Semina ya kuadhimisha miaka 60 ya Tanzania kupokea wakimbizi nchini, semina iliyofanyika jijini Arusha. |
PICHA: Baadhi ya washiriki wa semina na maandalizi kitabu cha miaka 60 ya Tanzania kupokea wakimbizi wakimsikiliza waziri Simbachawene ayupo pichani. |
PICHA: Mkurugenzi wa shirika la DIGINITY KWANZA, Bi Janemarry Ruhundwa, akitoa risala kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, ambapo aligusia kuhusu Tanzania inavyojali haki za wakimbizi kati ya nchi za maziwa makuu. |
PICHA:Washiriki wa mkutano wa kimataifa unaongazia wakimbizi nchini tanzania wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi waziri wa katiba na sheria hayupo pichani. |
PICHA: Antonia Jose Canhandula, Mkurugenzi wa shirika la wakimbizi nchini Tanzania akito hotuba yake kuhusu hali ya wakimbizi nchini. |
PHOTO: Washiriki wa semina ya kimataifa inaongazia wakimbizi nchini tanzania ambao walihidhulia pia kuweka mipango endelevu katika kuwahudumia wakimbizi pamoja na kuaandaa kitabu cha miaka 60 ya Tanzania kupokea wakimbizi. Picha zote na Samweli Mnguru. |
Post a Comment