PHOTO: 👆 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria
PHOTO: 👆 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakisalimiana na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakatiwakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyereretayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.
PHOTO: 👆 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameongoza na na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula wakielekea kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Myerere jijini Dar es salaam tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchihiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Mei, 2019 ameondoka nchini kwenda Afrika ya Kusini ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa nchi hiyo, Mhe. Cyril Ramaphosa.
Katika safari hiyo Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Wakizungumza kabla ya kuondoka, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg. Mangula wamesema Tanzania na Afrika ya Kusini zina uhusiano mkubwa na wa kihistoria na kwamba Serikali na chama zina kila sababu ya kudumisha uhusiano na ushirikiano huo.
Viongozi hao wameondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini, Mhe. Rais Magufuli atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia ambako pia atazindua mtaa uliopewa jina la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kutambua
PHOTO: 👆 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameongoza na na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula wakielekea kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Myerere jijini Dar es salaam tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchihiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria
Post a Comment