0
ARUSHA.
PHOTO: Kutoka kushoto ni Abdul Omar Maziku mwezeshaji (katikati) Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro (kulia) Frank Malulu  ambaye ni mwezeshaji.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Ndg. Gabriel Daqqaro amefunga mafunzo mafupi ya siku nne ya matumizi ya vifaa vya kieletroniki ela kwa mahofisa wa taasisi za serikali nchini mkoani Arusha.

Akifunga mafunzo hayo amesema, wahitimu hao wanapaswa kutumia mafunzo waliyopata kuitumimia jamii kwa haki pamoja na kuwaona wao ndiyo sehemu ya utendaji wao.

Pia amegusia sualaa Rushwa kwa watendaji hao kutoka idara tofauti za serikali ikiwemo hospitali, mahakama kwa kutoyimiza wajibu wao ili kuepuka kupata adhabu kali watakayopewa.

"Mnamtendea mwananchi haki kulingana na hitaji lake pasipo kupokea rushwa mtakuwa mnafanya jambo kubwa sana, ukizingatia Rais John Pombe Magufuri anasisitiza haki kwa mwananchi pasipo rushwa" amesema DC Daqqaro.

Hata hivyo amesisitiza watumishi wenye vyeti vya kufoji kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuwepo utendaji wenye weledi kwa watumishi wanaopata nafasi ya kuwatumia wananchi.

PHOTO: Picha ya pamoja ya wakufunzi na wahitimu wa mafunzo ya mfumo wa kieletroniki waliokaa pamoja na nkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqqaro (wa pili kutoka kulia waliokaa)

"Endapo mtatumia mfumo huu wa kieletroniki vizuri hauwezi kukupa uchovu na kukufanya kuchoka pale mwananchi anapokuja kutaka huduma kwenye nafasi yako" aliongeza DC Daqqaro.

Vilevile amewataka wahitimubwa mafunzo hayo kutunza usiri wa taarifa za mtu yeyote ili kuepusha mgongano wowote ikiwa ni pamoja na usiri kwa serikali.

Mafunzo hayo yametolewa wakufunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma cha Tabora hii ikiwa sehemu mojawapo ya mkakati wa serikali katika kuwapa elimu watumishi juu ya mfumo wa kieletroniki ni moja ya sehemu ya serikali katika kuhakikisha taasisi zake zinakuwa salama na kuunganishwa kwenye e-Nert.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top