ARUSHA.
Mkurugenzi
mkuu wa CRDB nchini Dr. Charles Kimei amewata wanahisa wote wanaotarajia
kushiriki mkutano mkuu wa 23 wa mwaka wa benki ya crdb unaotarajia kufanyika siku ya
jumamosi jijini Arusha tarehe 19.05.2018, kuhudhulia kwa wingi ili kujua maendeleo ya benki yao, pamoja
kujua kujua namna ya kuwalithisha ndugu Hisa.
PHOTO: Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Dr.
Charles Kimei akiongea na wanahabari juu ya mkutano mkuu wa wanahisa wa benki
ya crdb jijini Arusha.
|
PHOTO: Waliokaa mbele ya Wanahabari ni viongozi wa CRDB katika ni Mkurugenzi wa CRDB Dr. Charles Kimei akiongea nao, kushoto Jadi Ngwale na kulia ni James Mabula. |
Picha zote na Leonard Mutani.
HABARI ZAIDI.
Akiongea
katika mkutano na wanahabari leo jijini Arusha Dr. Kimei amesema benki ya CRDB
wanajivunia kuwa benki ya kwanza kuwa na wanahisa wanahudhulia mkutano wao wa
mwaka kwa wingi wapatao 1500 ambayo ni asilimia 75% hapa nchini.
Mkutano
huo unatarajiwa kutoa nafasi kwa wanahisa wote kupokea taarifa kutoka wa
wakurugenzi wa bodi ambao ndiyo wenye jukumu la kusimamia shughuli za benki kwa
mwaka unaohusika kama masuala ya kifedha.
Katika mkutano huo
mwanahisa yeyote ambaye hataweza kuhudhilia mkutano mkuu huo anaweza kuwakilishwa
na ndugu, jamaa au mfanyakazi wa benki ya CRDB ili kuweza kupiga kura, kutoa
maamuzi kuhusu maendeleo ya benki.
Vilevile Dr. Kimei
amesema benki ya CRDB ilipata faida ya shilingi 36bilioni kwa mwaka uliopita
pamoja na changamoto mbalimbali zilizokuwepo.
Pamoja na hayo Dr. Kimei
amejibu swali uliloulizwa ikiwa kupitia mkutano huu kama atawaaga wanahisa
ndani ya Benki hiyo Dr. Kimei amesema “Huu siyo mkutano wangu wa mwisho kuwaaga wanahisa,
contract yangu inaisha mwezi mei mwakani, kwa hiyo mwezi mei naweza kupata
nafasi ya kuwaaga wanahisa.”
Akielezea hali ya
mikopo ndani ya benki hiyo, amesema hali ya mikopo imekuwa ni mbaya kutokana
kwa mwaka jana, maana hata kanuni za kutunza mahesabu na kanuni za kutenga tengo
la mikopo chechefu imebaridika kutokana mfumo mpya wa kimataifa wa ifrars no 9.
Mfumo huo mpya unataka
unapotaka kutoa mkopo lazima utenge bajeti yake kwanza kabla ya kutoa, ili
uweze kuangalia kama mkopo huo unaweza kulipika au hautaweza.
Post a Comment