ARUSHA.
![]() |
PHOTO: Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheli
nchini Dkt. Fredrick Oneal Shoo akifungua
mkutano kwa hotuba jijini
Arusha.
|
Mkutano mkuu wa Halmashauli ya
makanisa duniani (WCC) unafanyika jijini Arusha ambapo Umishionali na Uinjilisti
duniani kila wakati unakusanya kwa pamoja makanisa na madhehebu kutoka pembe za
dunia ili kujadili, kutafakari na kupeana uzoefu kutokana na Imani
inavyosambaa.
Katika mkutano huo unaofanyika
nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958,ikiwa ni kila baada ya
muongo na unafanyika ikiwa ni kila dhehebu kushirikiana katika ujuzi na
majadiliano ya kidini.
Aitha kufanyika kwa
mkutano huu hapa nchini, utazingatia changamoto na mbegu za fursa za Afrika ya
leo, kwamba inawezaje kuunda teolojia ya utume na mazoezi ya baadaye na jinsi
gani Afrika inaweza kuongeza uelewa wa ujumbe kwa namna ya kipekee na ya
kibunifu.
Hizi hapa chini ni baadhi ya picha za matukio
yaliyojili kwa siku ya leo kutoka Ngurdoto Mountain Lorge jijini Arusha.
![]() |
PHOTO: Maandamano
kuelekea kufungua mkutano yakiongozwa na Mchungaji Dkt. Fredrick Shoo kuelekea
kwenye ukumbi wa mkutano uliopo kwenye Ngurdoto Mountan Lodge.
|
![]() |
PHOTO: Baadhi ya wahudhuliaji wa mkutano huo wakisikiliza na kuangalia nyimbo zilizokuwa zikiimbwa katika mkutani huo. |
![]() |
PHOTO: Kikundi cha
kusifu na kuabudu kikiimba wakati wa kuanza kwa ibada ya pamoja wakati wa
ufunguzi wa mkutano huo.
|
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.