BURUNDI.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza pichani chini (kushoto) ametangazwa na chama
chake kuwa ni kiongozi wa kudumu na mahiri asiyelinganishwa na yoyote.
![]() |
Profile PHOTO: Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kushoto) akivishwa
nishani.
|
“Ninatumia fursa hii kutangazia waliojariwa kufika hapa kuwa
kamati kuu ya chama chetu cha CNDD FDD imechukuwa hatua kuwa mheshimiwa rais wa
nchi yetu Pierre Nkurunzinza ndiye wa kwanza, ni kiongozi mahiri kwetu, ni
mzazi anayetushauri, asiyelinganishwa na mtu yoyote.Ninaomba wafuasi wa chama
chetu kuheshimisha hatua hii’’ alisema Evariste
Ndayishimiye katibu mkuu wa chama tawala Burundi cha CNDD FDD siku ya Jumamosi
akiwa tarafani Mwumba katika mkoa wa nyumbani kwa rais Nkurunziza.
Ilikuwa katika sherehe za kukamilisha kile
kilichofahamika kama mashindano ya kitamaduni yaliyoandaliwa na chama cha CNDD
FDD.Lakini katibu mkuu wa chama cha CNDD FDD hakufafanua zaidi maneno hayo na
athari yake kwa utawala wa nchi.
Post a Comment