ARUSHA.
*Kikao cha
mendeleo na kamati ya ushauri cha mkoa wa Arusha kimekaa na kujadili mapitio na
maazimio ya mkoa. Mwenyekiti wa Kamati ya ushauli wa mkoa ambaye ni mkuu wa
mkoa wa Arusha Gambo amewakilishwa na mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Hassan
Kimanta.
![]() |
PHOTO: Mkuu wa wilaya ya Monduli Idd Hassan Kimanta
akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye hakuwepo katika mkutano huu.
|
HABARI
KWA UNDANI.
Kikao hiki ni maalum kupitisha bajeti
ya mkoa ili kufikia maendeleo kwa mwaka wa fedha unaotarajia kuanza kwa Halmashauli zote za mkoa wa Arusha kwa
mwaka 2018/2019.
Hata hivyo Mwenyekiti amezitaka
halmashauli kuongeza ukusanyaji wa mapato, kutoka asilimia 57% kwa mwaka
unaomalizika 2017/2018 ili kufikia malengo. Amezikata halmshauri kufikia mwezi
juni mwaka huu kila wilaya ifikie makusanyo ya mapato kwa asilimia 100%, ili kuwasaidia
wananchi katika maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Bw. Kimanta amewataka
watendaji wa serikali kusimamia huduma muhimu kama Maji, Afya na Elimu ili kuendana na sera ya
serikali ya kuwaletea wananchi huduma zilizo bora hasa huduma za maji vijijivi,
kwani maji, elimu ni vitu muhimu kwa kila mwananchi wa mkoa wa Arusha.
Kwa
upande mwingine amewaomba wanahabari kwa kusema “ninyi ni wadau wa mkoa wa Arusha, pamoja na kutoa
habari muangalie ni habari haina gani mnayotoa kwa wananchi isiwe habari ya
kichochezi, muwasaidie viongozi kutoa habari za maendeleo ikiwemo vivutio
vinavyoweza kufanya mkoa uvutie wawekezaji ili jiji letu liweze kuendelea
kupitia habari ambazo mnatoa”
Pamoja
na wajumbe kumuomba mwenyekiti kusaidia majimbo mbalimbali, mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari
amemuomba mwenyekiti kuwasaidia wakazi wa jimbo lake la Arumeru mashairiki
waliokuwa wakilima bangi kama zao lao la biashara kwa ajili ya kujipatia kipato
na kuwapatia zao mbadala litakalowasaidia kuwapatia kipato kwa ajili ya kujikimu
na kuendeleza maisha yao ya kila siku.
Mbunge wa Monduli ameitaka serikali kuacha kuzuia ruzuku ili halmashauli zifikie malengo ikiwa ni pamoja na kuangalia namna mapato yanayokusanywa kwenye halmashauli hizo ziweze kubaki na kusaidia maendeleo sehemu husika.
![]() |
PHOTO: Baadhi ya wabunge wa mkoa wa Arusha,
kutoka kulia, Godbless Lema –Arusha mjini, Julius Karanga –Mbunge wa Monduli na Joshua Nassari –Arumeru wakifuatilia.
|
![]() |
PHOTO: Baadhi ya wachungaji waliohudhulia mkutano wa bajeti ya mkoa wa Arusha wakifuatilia.
|
![]() |
PHOTO: Baadhi wa maofisa wa usalama wa kamati
ya mkoa waliokuwepo kusikiliza na mstakabali mzima wa mkoa wa Arusha.
|
![]() |
PHOTO: Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari –Arumeru akichangia katika hoja kwa upande wa jimbo lake, (kushoto) Mbunge wa Monduli Julius Karanga akimsikiliza Nassari.






Post a Comment