0
PWANI
ELIMU HAINA MWISHO.
Mahafari ya kumi na mbili (12) ya Shule ya sekondari ya Baobab iliyopo mkoani pwani wilaya ya Bagamoyo yamefanyika shuleni hapo ambapo mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri ofisi ya Nchini, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jaffo.

PHOTO: Waziri wa Naibu Waziri ofisi ya Nchini,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
Suleiman Jaffo akiongea na kadamnasi wakiwemo
wahitimu wa kidato cha sita.
Katika mahafari hayo ambayo wahitimu wapatao 295 wanatarajia kuhitimu elimu yao ya kidato cha sita katika shule hiyo.

Shule ya sekondari Baobab inayomilikiwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Shajar School Association ilianzishwa mnamo mwaka 2005 ikiwa na wanafunzi 70 wa jinsia ya kike pekee ambapo baadae uongozi ulifanya mabadiriko na kuamua kuifanya kuwa mchanganyiko.

Katika sherehe za mahafari hayo Uongozi wa shule hiyo umeiomba serikali kurekebisha sheria ya aridhi namba 178 ili iruhusu kubadirisha matumizi ya aridhi lakini pia Serikali iiwezeshe mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kutunisha mfuko wa kutoa huduma za mikopo na vifaa kwa shule za serikali na binafsi ili kuwepo maendeleo makubwa ya Elimu nchini.

Hata hivyo naibu Waziri Suleiman Jaffo pamoja na kuhusifu uongozi wa shule hiyo kwa mafanikio wanayopata kutokana na ubora na elimu wanayotoa shule iyo, amewataka kuweka nafasi stahiki kwa mzazi yeyote kuweza kumleta mwanaye pasi kuwepo vipingamizi.

Katika kujibu risala iliyotolewa kwake amesema, serikali ipo bega kwa bega na sekta binafsi katika maendeleo ya Elimu nchini na ndiyo maana inaendelea kutoa fulsa kwa Mtanzania mwenye uwezo wa kuwekeza kwenye sekta hiyo.

"serikali tutaangalia ni jinsi gani tunaweza kuzisaidia mamlaka zinazohusika na elimu kama TEA kuweza kufanikisha malengo ya kunyanyua elimu yetu nchini" alisema Suleiman Jaffo.


Kwa upande mwingine mdau wa elimu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Esther Alexanda kutoka Manyara ambaye pia ni mwenyekiti wa shule binafsi nchini ameiomba serikali wawekezaji kupitia elimu hawaleti mvutano ktk nyanja hiyo bali wanaomba ifanye Public Private Partnership (PPP) "kwenye sekta ya Elimu kama ilivyo kwenye sekta ya Afya ili kuwepo na maendeleo kwa upande huo"

PHOTO: Naibu waziri (Tamisemi) Suleiman Jaffo (katikati), Mkurugenzi mkuu wa shule za Baobab (kulia) na viongozi wengine wakiimba wimbo wa taifa wakati wa sherehe hizo.

PHOTO: Mdau wa elimu ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Esther Alexanda kutoka Manyara
PHOTO: Mkurugenzi mkuu wa shule za Baobab akiongea wakati wa sherehe hizo na kabla hajamkaribisha naibu waziri wa Tamisemi Suleimani Jaffo (pichani kulia) 
PHOTO: Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikillza Mkurugenzi mkuu wa shule hizo (pichani juu) akiongea kwenye sherehe hizo.
PHOTO: Wahitimu wa kidato cha sita wakisoma risala yao kwa naibu waziri wa Tamisemi (hayupo pichani)
PHOTO: Mkurugenzi mkuu wa shule za Baobab akimkakabidhi naibu waziri wa Tamisemi Suleimani Jaffo (kulia) risala ya shule.



PHOTO: Naibu waziri (Tamisemi) Suleiman Jaffo (katikati) akiongea mara baada ya risala iliyosomwA kwake.

PHOTO: Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikillza Naibu waziri Suleimani Jaffo (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba kwa wanafunzi, ndugu, jamaa, walimu waliofika katika sherehe hizo.



PHOTO: Naibu waziri (Tamisemi) Suleiman Jaffo (aliyeshika kipaza sauti) akiwatunuku vyeti wanafunzi wanaohitimu elimu ya kidato cha sita, pichani chini. 
PHOTO: Baadhi ya wahitimu wakinyanyua juu vyeti vyao kuonyesha furaha ya kuhitimu elimu ya sekondari wkt wa kukabidhiwa na naibu waziri shuleni hapo Bagamoyo Mkoani Pwani.





Post a Comment

 
Top