0
MBEYA
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Mbeya Michael Mteite ambaye alisoma hukumu siku ya leo, amemuhukumu Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi pamoja na Katibu wa Kanda ya Nyasa (CHADEMA) Emmanuel Masonga kwenda jela kutumikia kifungo cha miezi mitano (5)

ILIVYOKUWA.
Mbunge Joseph Mbilinyi maarufu SUGU alisema "Mhe Rais Magufuli hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa Jela miezi minne Lema, kumteka Ben saanane, kumteka Roma na kumzuia SUGU asiongee"

Sugu na Masonga walishtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba30 mwaka 2017 wakiwa viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya

PHOTO: Prof. Abdalah Safari (katikati) akiwana viongozi wenzake wa Chadema (kushoto) ni Mbunge Joseph Mbilinyi kabla ya kutolewa hukumu.


PHOTO: Wabunge wa Chadema (kulia) MP Msigwa (kushoto) Mbunge wa Arusha Godbless Lema na viongozi/ wanachama wengine  wa Chadema waliofika mahakamani mapema leo.

PHOTO: Wabunge wa Chadema (kulia) John Mnyika na wabunge wengine wa CDM waliofika mahakamani mapema leo.




Post a Comment

 
Top