0
>>PHOTO: George Opong Wear akila
Kiapo mbele ya Jaji wa mahakama
kuu nchini Liberia Francis Korpor
(anayeonekana mgongo)
LIBERIA.


Nyota wa zamani wa soka George Weah ameapishwa leo kama rais wa Liberia mbele ya maelfu ya wafuasi wake, ikiwa ni zoezi la kwanza la kukabidhiana madaraka kati ya marais wawili waliochaguliwa na wananchi nchini Liberia tangu 1944.
George Weah ameapishwa majira ya mchana mbele ya Mkuu wa Mahakama Kuu Francis Korpor, katika uwanja mkubwa wa mpira kwenye mji mkuu wa Monrovia, ulifurika wananchi na watu mbalimbali waliofika kushuhudia sherehe hizo za kipekee nchini humo.
Akihutubu wananchi na wageni mara baada ya kula kiapo, Weah amesema:"Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."
>>PHOTO: George Opng Wear akiwa amekalia kiti ambacho ni ishara ya kurithi amdaraka makubwa makubwa nchini Liberia (kushoto) ni mkewe.

Aliongeza kuwa “nimekuwa katika viwanja vingi, lakini sijawahi kuhisi hivi” George Weah anamrithi Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza aliyechaguliwa kushika nafasi ya urais barani Afrika mnamo mwaka 2005.
Maelfu ya raia wa Liberia wakiwemo marais kadhaa hasa kutoka Afrika Magharibi wamehudhuria sherehe hizo, wakiwemo wacheza kandanda kama Didier Drogba na Samwel Eto'o ambao ni miongoni mwa wengine wamehudhuria sherehe hiyo.
>>PHOTO: Samwel Etoe (aliyenyoosha mkono) ni miongoni mwa wanasoka waliokuwepo katika sherehe hizo za kuapishwa George
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mchezaji huyo zamani wa mchezo wa soka, alisema kazi yake kubwa itakuwa ni kuhimiza amani nchini humo. Kuapishwa kwa Weah kunamaliza, uongozi wa rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2005.
Bi.Sirleaf anaondoka akiwa na rekodi nzuri ya kuhimiza amani nchini humo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu wengi.

Post a Comment

 
Top