ARUSHA.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya
Meru mkoani Arusha Simon Kaaya ameonya walimu wote waliopo wilayani humo
kufuata sheria na taratibu zinazotolewa ili kwenda sambamba na kauli za
maendeleo zinazotolewa na viongozi wanao iongoza serikali iliyopo madarakani chini ya Chama cha Mapinduzi CCM.
PHOTO: Mwenyekiti wa
Jumuiya ya wazazi wilaya ya Meru Simon Kaaya akiogea na wanachama, viongozi
wa CCM (hawapo pichani) Kulia ni katibu wake.
Katika ziara ya siku moja iliyowafikisha katika shule mbili zilizozopo wilayani humo, mwenyekiti huyo amesema kuwa elimu inayotolewa sasa bado haijakidhi malengo chanya yatakayoleta mabadiriko makubwa wilayani humo, "kumekuwa na baadhi ya walimu ambao wamekuwa na tabia ya kutofanikisha ratiba ya masomo kwa mwaka mzima." Simon Kaaya ameongeza kuwa "sisi kama viongozi tunaosimamia serikali iliyopo madarakani, tutahakikisha mabadiriko makubwa yanayofanywa na serikali yanafanyika katika ngazi zote hasa upamse wa elimu" Mwenyekiti huyo anayefahamika kama "mwenyekiti kijana" amepigilia msumari kwa walimu wa shule zote za serikali wilayani humo yeyote atakayekiuka na kuchangisha wazazi pesa atachukuliwa hatua. Kwa upande mwingine ameweka uzito suala la maadili hasa kwenye uvaaji wa mavazi kwa vijana wa kike na kiume, "walimu hakikisheni vijana wa kike wanavaa sketi zenye urefu chini ya magoti na wavulana wasivae suruali zilizobana (maarufu kama chupa) ili kujenga jamii yenye tabia njema na kujua utamaduni wake" Pamoja na hayo, wilaya hiyo imekumbwa na uharibifu wa mazingira kwa wavamizi wanaochimba mchanga, kukata miti na kupasua mawe pasipo kufuata sheria, hivyo ameonya suala hilo analifanyia kazi kwa kutoa kauli na kuwataka yeyote anayefanya shuguli za aina hiyo aache mara moja, "sheria kali zipo tayari kutumika kwa yeyote atakayekamatwa" |
Post a Comment