DAR ES SALAAM.
*********************************************************
Mkuu
wa wilaya ya Temeke Jijini Dar Es Salaam Mh. Felix Lyaviva amewataka wanafunzi wapatao 300 wanaosoma
katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa masomo ya ununuzi na ugavi wanaotarajia
kuwa watumishi katika nyanja hiyo kuhakikisha wanatumia vyema fedha
zinazotolewa na serikali kwa lengo la manunuzi.
PHOTO:
Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaviva (katikati) akiwasili na kupokelewa na kaimu mkurugenzi
wa PSPTB, Godfred Mbanyi (wa pili kulia) na wa chuo cha TIA alipowasili chuoni
hapo.
|
PHOTO:
Sehemu ya wanafunzi waliohudhulia mafunzo wakimsikiliza kaimu mkurugenzi mkuu wa PSPTB (pichani chini) alipokuwa akiongea nao.
|
PHOTO Juu na Chini:
Kaimu
mkurugenzi wa ununuzi na ugavi nchini Godfrey Mbanyi akiongea na wanafunzi wa
chuo cha taasisi ya uhasibu nchini TIA kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
|
PHOTO:
Baadhi ya wanafunzi waliohudhulia mafunzo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya
temeke Mh. Felix Lyaviva alipokuwa akitoa hotuba, (pichani chini).
|
PHOTO:
Mkuu wa wilaya Mh. Felix Lyaviva akiongea na wanafunzi waliokuwa katika mafunzo.
|
PHOTO:
Kaimu
mkurugenzi wa psptb Godfred Mbanyi (kulia) akimuangalia DC Felix Lyaviva (aliyesimama) alipokuwa alitoa hotuba katika kabla ya kuanza kwa mafunzo
hayo.
|
SOMA ZAIDI/Read more….
Katika hafla fupi ya
kufungua mafunzo hayo mkuu huyo wa wilaya amesisitiza kumuunga mkono Rais John
Pombe Magufuri katika jitihada zake kuondoa ufisadi, wizi na kulinda rasilimali
za nchini ili ziweze kuwasaidia wananchi na kuondokana na changamoto ambazo
zimekuwa zikiwakabili.
DC Felix Lyaviva alisema “nyie msipowatendea
haki hawa watanzania mtakuwa mnamuangusha Rais wetu, na sisi wasaidizi wake
hatutakubali, mimi sitaangalia kama ni afisa ugavi uliyesajiliwa, maadamu
unaiujumu nchi yangu, nitahakikisha nakuchukulia hatua pamoja na kushitakiwa
ikiwezekana na kuuhujumu uchumi”
Hata hivyo mafunzo hayo
yamefanyika ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwaongezea wanafunzi hao ili kuweza
kuwa na uelewa wa ununuzi na ugavi katika
vitengo mbali mbali vya serikali.
Mkuu wa wilaya
aliwataka wahitimu hao wa mafunzo kuhakikisha wanazingatia maadili ya kazi yao
katika manunuzi ya fedha ya serikali ambayo inatengwa kwa kiasi cha asilimia 75
kwa ajili manunuzi na ugavi.
Post a Comment