0
ARUSHA.

Naibu waziri wa fedha na mipango Dr. Ashantu Kijaji amepiga marufuku kwa wafanyabiashara na wananchi wanaotoza huduma kwa kutumia muamala wa fedha za kigeni wakati alipokutana na wafanyabiashra na wadau wa sekta ya utalii jijini Arusha katika hatua ya kushikamana na kuwasikiliza wadau hao ikiwepo kero mbalimbali za kodi.

PHOTO: Naibu wa waziri wa fedha na mipango Dr. Ashantu Kijaji akiongea na wafanyabiashara na wadau wa sekta ya utakii (hawapo pichani) mapema leo jijini Arusha.

PHOTO: Baadhi ya wafanyabiashara na wadau wa sekta ya utalii wa jijini Arusha wakimsikiliza Naibu waziri wa fedha na mipango (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hotuba.
PHOTO: Dr. Ashantu Kijaji (aliyesimama) akiongea na wafanyabiashara, wadau wa sekta ya Utalii (hawapo picha) aliyekaa kulia ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akisikiliza kwa umakini.



HABARI KWA UNDANI.
Katika mkutano huo ambao wadau hao wa sekta ya utalii waliomba kupunguzwa utitiri wa kodi unaotokana na baadhi ya taasisi mbalimbali zinazokusanya kodi kuangalia namna gani kutakuwepo na njia stahiki ya ukusanyaji wa namna moja.

Hata hivyo Dr. Ashatu Kijaji amewataka wadau hao kuendelea kuiamini serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuri yenye dhamira ya kutokuwepo kwa Mtanzania yeyote anayeathirika na mfumo wa kodi au ushuru katika Taifa hili.

Kwa upande mwingine ametoa angalizo juu ya matumizi ya pesa za kigeni hasa dola ya marekani kuwa, kumekuwepo na baadhi ya mashirika kutumia fedha hiyo huku uchumi ukirudi nyuma kutokana na fedha ya ndani kutotumika.

Dr. Kijaji amesema “matumizi ya fedha ya kigeni yanasimamiwa na sheria mbili, sheria ya kwanza ni ya usimamizi wa fedha za kigeni ya mwaka 1992 na sheria ya pili ni ya Benki kuu ya Tanzania ya 2006 na tamko la serikali la mwaka 2007, sheria zote hizi azizuii matumizi ya fedha za kigeni”

Vilevile sheria hizo mbili zinaruhusu matumizi ya fedha za kigeni bado sheria haijaona umuhimu wa matumizi ya fedha hizo kutokana na nchi kuwa na fedha yake kwa matumizi na kuwepo kwenye mzungumko wa fedha.

“Sarafu ya Tanzania ndiyo fedha halali kwa malipo ya ndani ya taifa letu na ndiyo fedha halali kuthaminisha thamani ndani ya taifa letu” alisema Dr. Ashantu Kijaji.

Baadhi ya wafanyabiashara nchini wamekuwa wakitoza kwa dola na bei tofauti tofauti na inayotambuliwa na benki kuu, serikali imeamua kuweka utaratibu mpya na ambao unakuwa ni sheria hapa nchini kwa kutoza huduma zote kwa kutumia thamani ya shilingi ambapo tamko hilo linakuwa ni sheria kuanzia sasa.

Dr. Ashatu Kijaji ameendelea kusema”bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania,bei hizi zinajumuisha kodi za nyumba za kuishi, ofisi,aridhi, elimu, afya, vyombo ya usafiri na vifaa vya kieletronik”

Hata hivyo kwa wageni watakaokuwa tayari kulipa huduma kwa fedha ya kigeni wanaweza kufanya hivyo pasipo kulazimishwa, na ametoa angalizo kwa wafanyabiashara watakaotoza huduma kwa fedha za kigeni kuwa watakuwa wamefanya kosa “na sheria itakuwa imechukua mkondo wake”

Post a Comment

 
Top