LIBERIA.
PHOTO: Rais Ellen Johnson Sirleaf |
Chama kinachotawala nchini
Liberia, cha Unity party, kimemfukuza rais anayemaliza muda wake baada ya uchaguzi nchini humo bi Ellen Johnson
Sirleaf kutoka kwenye uanachama.
Chama hicho kilipiga kura ya kumfuta uanachama siku ya
Jumamposi na hatua hiyo ilichukuliwa baada ya tuhuma kwamba hakumuunga mkono
makamu wake wa urais Joseph Boakai aliyekuwa mgombea wa urais kwenye uchaguzi
uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Boakai, ambaye alikuwa makamu wa rais kwa miaka 12,
alishindwa katika kinyang'nyiro cha urais na nyota wa zamani wa soka, George Waeh.
Johnson Sirleaf, ambaye ni mshindi wa tuzo la amani la
Nobel, hakuwa na nafasi ya kugombea tena urais kutokana na katiba ya Liberia kutoruhusu kufanya hivyo.
Wakosoaji wa Boakai walimshutumu kwa kile walichokiita
"kutofanya mengi ya kuimarisha taifa" akiwa makamu wa rais.
Iwapo kila kitu kitaenda
shwari, Liberia itashuhudia ubadilishanaji mamlaka kwa njia ya kidemokrasia kwa
mara ya kwanza katika kipindi cha Zaidi ya miaka 70 iliyopita.
Source: VoA
Post a Comment