0
ARUSHA.

Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wajiuzulu.
Madiwani hao wa kutoka halmashauri ya wilaya ya Longido wameamua kujiuzuru na kurudi kwa mzazi wao ambaye ni chama cha Mapinduzi -CCM.

Taarifa iliyotolewa leo na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa wilaya ya Longido Juma Mhina inawataja madiwani hao kuwa ni Diyoo Lomayani Laizer kata ya Olmolog, Jacob Silas Mollel kata ya Elang'atadapash na Elias Mepukori Mbao wa kata ya Kmawaga.

Sababu za kujiuzulu madiwani hao wamezieleza kuwa ni kumuunga mkono Rais Magufuri katika vita dhidi ya ufisadi, kurejesha nidhamu kazini na kuinua uchumi wa nchi.

Mkurugenzi huyo alisema "“tayari tumepokea barua zao na tumezipeleka tamisemi kwa ajili ya taratibu za kisheria ili kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi mdogo baada ya tume kupata taarifa hii"

Katika taarifa nyinge, aliyewahi kuwa mbunge wa longido Onesmo Nangole amethibitisha kujiuzulu kwa madiwani hao na kusema chama kinafuatilia kujua kwa undani.

Post a Comment

 
Top