ARUSHA.
Jeshi
la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani Arusha kimefanya mkutano na
wamiliki wa shule binafsi zinazojulikana katika muungano wao wa TAMONSCO kanda
ya kaskazini katika hatua ya kuangalia usafiri wa mabasi ya wanafunzi
unaotumika kuwasafirisha wanafunzi kwenda na kutoka shule.
PHOTO: Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani
mkoani Arusha (RTO) J.Bukombe akiongea na wamiliki wa shule binasfi (pichani
chini) alipokuwa akisisitiza jambo mapema leo jijini Arusha.
|
PHOTO:
Baadhi wa wamilikiwa shule binafsi za jijini Arusha wakimsikiliza kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani (pichani juu)
|
PHOTO:
Meza kuu ya viongozi waliokuwa wakisimamia na kuendesha mkutano huo uliofanyika
katika bwaro la maofisa wa jeshi la polisi jijini Arusha.
|
PHOTO:
Viongozi wa shule binafsi za kidini wakifuatilia na kuandika mambo muhimu
yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo.
|
HABARI
KWA UNDANI.
Katika mkutano huo
uliowakutanisha viongozi wa jeshi la polisi ukiongozwa na kamanda wa kikosi cha
usalama barabarani mkoa wa Arusha (RTO) JC. Bukombe mkoa wa Arusha na upande wa
wamiliki wa shule hao ukiongwa na mwenyekiti msaidizi wa shule binafsi kanda ya
kaskazini/magharibi Bi. Sofia Hamed Okash.
Aitha mkutano huo jeshi
la polisi limetoa onyo kwa wamiliki wa shule hizo kutumia magari ambayo hayana
na hayakidhi vigezo na yasipakwa rangi
ya njano pamoja na kujaza wanafunzi kuzidi uwezo wa gari, sheria kali ikiwepo
kukamatwa kwa magari hayo na kuchukuliwa hatua stahiki.
Katika hatua nyingine
jeshi hilo limetoa nafasi mwishoni mwa wiki ya tarehe 27 na 28 wamiliki wote wa
magari yanayobeba wanafunzi kuyapeleka magari yao kwa ajili ya ukaguzi na
kupewa stika kuonyesha kuwa gari hiyo itakuwa imefanyiwa ukaguzi na kuruhusiwa
kubeba wanafunzi.
Hata hivyo kamanda
Bukombe ameonya kwa wamiliki watakaotumia njia ya panya ili wapate stika pasipo
kukaguliwa ikifahamika udanganyifu huo kufanyika jeshi la polisi halitasita
kumchukulia hatua mmiliki wa shule ambaye gari lake limehusika.
Post a Comment