0
NAIROBI.
Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) Tundu Lissu ametoka kwenye hospitali ya Nairobi nchini Kenya mapema leo asubuhi kisha kukwea ndege na kuelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

PHOTO: Tundu Lissu (aliyekaa) akizungumza na waandishi wa habari mara alipotoka kwenye hospitali ya Nairobi tayari kusafilishwa kuelekea nchini Ubeligiji kwa matibabau zaidi.

HABARI KWA UNDANI.

Baada ya kazi kubwa  ya kuurejesha mwili wake na kuweza kutengemaa kufikia hali yake ya kawaida, Mbunge huyo ameondoka majira ya 2.30 asubuhi ya leo jumamosi kwa ndege ya shirika la Kenya ambapo ameambatana na mkewe Alicia.

Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma. Mwanasiasa huyo alisindikizwa mpka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na wanae mapacha Augustino na Edward, ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.

"Nawashukuru sana madaktari wa hapa Nairobi na wale wa Dodoma wakiongozwa na Katibu Mkuu (wa wizara ya afya Profesa Mpoki Ulisubisya waliookoa maisha yangu, nakwenda Ubelgiji kwa matibabu, nikirudi mapambano yanaendelea, nawashukuru nyote mlioniombea, nawashukuru Wakenya na serikali yao ambao kwa miezi minne nikiwa hapa walinipa ulinzi wakati wote." Amesema Tundu Antipas Lissu.

Vilevile ameongea kwa msisitizo mbele ya wabunge na wanachama wa Chadema waliokuwapo akiwataka kuchapa kazi wakati yeye akiwa kwenye matibabu na kuwaahidi pale atakaporudi ataendeleza pale alipoishia.

Post a Comment

 
Top