DAR ES
SALAAM.
Chama cha ACT Wazalendo
kimefanya mkutano na wanahabari mapema leo na kubainisha kuwa chama hicho
kinafanya mikutano ya ndani na viongozi wa vyama vingine nchini ikiwa ni njia
mijawapo ya kuungana na kupigania demokrasia nchini.
PHOTO: Katibu
wa Itikadi, uenezi na mawsiliano kwa umma Ado Shibu akiongea na wanahabari
makao makuu ya ACT Wazalendo jijini Dar Es Salaam.
|
SOMA ZAIDI.
Akizungumza na wanahabari katibu
wa itikadi, uenezi na mawasiliano kwa umma Ado Shaibu amesema desturi ya
taasisi mbalimbali za kijamii zikiwepo za kisiasa ni kutoa muelekeo wa taasisi
kwa kila mwaka mpya unapoingia.
Katika mkutano huo Ado
amebainisha kuwa demokrasia ya kweli sharti ianzie ndani ya chama lakini ni
pale wanachama wanapopewa nafasi ya kushiriki kwenye maamuzi na kuchagua
viongozi wao kwa mujibu wa katiba ya chama husika.
“kamati kuu ya chama imeazimia kwamba mwaka 2018 uwe wa kuimarisha
usiriki wa chama chetu kwenye mapambano ya wafanyakazi. Pia chama chetu
kinatarajia kufanya kazi kwa karibu na vyama vya wafanyakazi ili kukabiliana na
kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi” alisema
Ado Shaibu.
PHOTO: Kutoka
kushoto; Hamad Taho –Katibu wazee ACT (katikati) Ado Shaibu na kulia Tumaini
Bigilimana –Diwani diwani jimbo la mhambwe na katibu wa madiwani mkoa wa
kigoma.
|
read more here...
Katika hatua nyingine
ACT Wazalendo kinaongeza ushirikiano maradufu na vyama vingine vya upinzani ili
kupigania demokrasia na katiba mpya, na kubainisha kuwa bila ushirikiano
madhubuti baina ya vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla.
Aliongeza kuwa “serikali ya
awamu ya tano imejipambanua bila soni kuwa hodari katika kuivunja misingi ya
demokrasia nchini, vita ya kuitetea na kuilinda misingi ya kidemokrasia haiwezi
kufanikiwa bila ushirikiano madhubuti baina ya vyama upinzani na wananchi kwa
ujumla”.
Aitha kiongozi wa chama hicho
cha ACT Zitto Kabwe ameshakutana na kufanya na mazungumzo ya awali na ndg Freeman
Mbowe mwenyekiti wa Chadema na ndg Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chauma ili
kuongeza mapambano ya demokrasia.
Post a Comment