NAIROBI.
Kwa mara ya kwanza nchi ya
Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangwa kurushwa
anga za juu mnamo mwezi Machi mwaka huu.
PHOTO Profile: Satelite
iliyoko angani ambayo ni
mfano wa ile ambayo nchi ya Kenya imeunda. |
Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi,
wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitenengeza
chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.
Setlaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya
kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo, setilaiti hiyo
yenye umbo la mche mraba ina ukubwa wa sentimita 10 za mraba - itajulikana kama
nano-setilaiti.
Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea
lakini ni wakenya wenyewe ndiyo walioitengeneza, Satelaiti hiyo
itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mwezi Machi na
kuzinduliwa rasmi kuizunguka dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.
Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa
mataifa mengine saba barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.
Mataifa mengine ni Misri, Afrika Kusini, Morocco, Algeria, Nigeria, Mauritius
na Ghana.
Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi
walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja
kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga
kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti
zao.
Source: BBC
Post a Comment