DAR ES SALAAM.
Ibada ya kumuapisha askofu mkuu wa kanisa la Anglican dayosisi ya Dar Es Salaam imefanyika jijini Dar Es Salaam kwenye kanisa la St. Alban Upanga.
PHOTO:
Askofu
mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Jacob Chimeledya akiongea wakati wa ibada ya
kusimikwa kwa Askofu mkuu wa jimbo la Dar Es Salaam
|
PHOTO: Rais John Pombe Magufuri
akisoma Biblia wakati wa kutoa hotuba mara baada ya kusimikwa kwa Askofu wa Jackson Sosthenes Jackson (kushoto)
aliyekaa.
|
PHOTO: Rais John Pombe Magufuri (kulia) akiendelea kusisitiza jambo kutoka kwenye Biblia (kushoto) aliyekaa ni Askofu wa Jackson Sosthenes Jackson.
|
PHOTO: Picha
ya pamoja Rais Magufuri, Rais Mkapa maaskofu waliokuwepo wakati wa Ibada ya
kusimikwa kwa Askofu Jackson.
|
HABARI KWA UNDANI.
Katika ibada iliyohudhuliwa na Rais John
Pombe Magufuri pamoja na mama Janeth Magufuri ilihudhuliwa pia na viongozi
mbalimbali wa kiserikali na viongozi wastaafu na wa madhehebu mbalimbali.
Kwenye hubiri lililotolewa na askofu
Donald Mtetemela ambaye ni Askofu mkuu mstaafu, amesema pamoja na mtu apendaye
nafasi ya uaskofu amechagua jambo jema lakini ni nafasi ambayo inachangamoto
kwenye utumishi.
Askofu Mtetemela alisema "ukiwa kiongozi unapaswa kuwa
na ngozi nene na wala siyo nyembamba, maana kuna mishale na maudhi
inayoweza kukuudhi"
Aliongeza kuwa kuna wengine wanaingia
kwenye nafasi ya uongozi wakitumia njia za nyuma au kwa kuruka ukuta. "hata daudi alikuwa
mwaminifu kwa Mungu lakini baadaye aliachwa"
Katika hatua nyingine askofu huyo
alizungumzia migogoro iliyopo kanisani na kunukuu ufunuo 12, kuwa hata shetani
alitamani nafasi iliyo juu dhidi yake, hivyo alianzisha migogoro
kwasababu ya tamaa ya madaraka na uongozi.
"hata mitume walikuwa na migogoro
kutaka kupandishwa vyeo, yatupasa kupambana kwanza ili baadaye upate taji
kwa kuwa kristo atakuvisha taji ya ushindi" alisema Mtetemela.
Amewataka waumini wa kanisa la Anglican
nchini kuacha tabia ya kila muumini kwenda kwenye ukumbi wa uchaguzi na majina
ya wale wanaowaona ndiyo wanaofaa kuwa viongozi, amesema kuwa "kila
mtu akija na jina lake sasa ni nani achaguliwe awe kiongozi".
Ameisifia serikali ya awamu ya tano chini
ya Rais Magufuri juu ya kukusanya kodi kuwa ni sehemu moja ya maandiko ili
kufikia hatua ya maendeleo ya kanisa na nchini.
NB. Itakumbukwa askofu aliyepita Valentina
Mokiwa alikuwa katika msigano wa kiuongozi kwa muda mrefu huku akikataa kuachia
madaraka pamoja na umri wake wa kustaafu ukiwa umefika ambapo ilipelekea
kukataa kutoka madarakani.
Post a Comment