0
Wanasayansi wanasema kwamba ziwa kubwa zaidi lenye maji tulivu barani Afrika Victoria linalounganisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, lipo katika hatari kubwa ya kukauka.

PHOTO: muonekano wa sehemu ya ziwa Victoria pembeni kukiwa na vyombo vya uvuvi. 
Wataalam hao wanasema kwamba uvuvi haramu na uliopitiliza pamoja na uvamizi wa mazingira kuzunguka maeneo ya ziwa hilo ni sababu kubwa inayohatarisha uhai wa ziwa hilo. 
Vilevile kuwepo kwa maji machafu na yanayotiririshwa kuelekea kwenye ziwa yanahatarisha usalama wa viumbe vya majini. Katika hatua ya kuhakikisha usalama na uwepo wa ziwa hilo Jeshi la Uganda limeweka mipango maalum ikiwa ni pamoja na kuharibu nyenzo za uvuvi zinazotajwa kuwa miongoni mwa sababu.


Source: BBC 

Post a Comment

 
Top