Kampuni kubwa ya pili kwa usafirishaji nchini kenya ijulikanayo kama fry 540 iimeanza kutoa huduma kati ya miji ya Dar Es Salaam na Nairobi nchini Kenya.
Hiyo ni moja ya hatua inayoongeza orodha ya mashirika ya ndege katika ukanda wa Afrika mashariki ambapo miongoni mwa vituo vinavyotazamiwa ni pamoja na miji ya Juba kwa sudani ya Kusini na visiwa vya Zanzibar.
Ndege hizo zitafanya safari tatu kwa wiki kutoka Nairobi mpaka Dar Es Salaam “Tunatarajia ndege mbili kusafiri kwa siku” alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji Nickson Ooko. Pia kuanza kwa safari kuelekea Tanzania inatarajiwa kuleta changamoto ya kiushindani kwenye nauli hasa kwa shirika la Kenya Airways.
Aliongeza kuwa “Ndege yetu ambayo huduma na bidhaa nafuu bila kusahau ubora, kwa mfano, hatutaweza kulipisha mzigo wa mteja wa ziada (extra luggage) mnyama (pet)”, pia inatazamiwa kutoa garama ya nauli ya kawaida toafauti na mashirka yaliyopo sasa.
Kamishina wa Tanzania nchini Kenya Angelina Musili alisema ndege hizo zitakuwa ni fulsa nyingine kwa sekta ya Utalii kati ya Tanzania na Kenya.
Post a Comment