NAIROBI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan, mara baada ya sherehe za kuapishwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, ambaye amelazwa jijini humo akipatiwa matibabu kutokana na majeraha kupigwa risasi.
Mama Samia ambaye aliwasili hospitalini hapo magharibi ya leo ambapo alimtakia kupona haraka nabkurejea nyumbani kuwatumikiwa wananchi, makamubwa Rais aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. Pindi Chana.
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu anakuwa ni kiongozi wa kwanza mkubwa kitaifa kwenda kumjulia hali mbunge huyo ambaye amelazwa hospitalini hapo tangu mwezi Septemba tarehe 7 mwaka baada ya tukio la kushambiliwa kwa kupigwa risasi na watu wanaosemekana hawajajulikana kufikia sasa.
Post a Comment