ARUSHA.
Mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi nchini (WCF) utafanya mkutano wake wa kwanza wa mwaka jijini Arusha kuanzia kesho.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Arusha mkurugenzi wa tiba na tathimini Abdulssalaam Omary amesema mkutano huo utakao toa taarifa ya mwaka mzima uliopita, pia wadau wataweza kutathimini maendeleo na changamoto zinazoukabili mfuko huo.
"katika mkutano huu mgeni rasmi anatarajia kutunuku tuzo kwa waajili waliofanya vizuri katika utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi" alisema Omary.
Vile vile wataalam mablimbali wenye uzoefu mbalimbali kutoka nchi kadhaa barani Afrika pamoja na shirika la kazi duniani (ILO) I'm wanatarajia kutoa mada katika mkutano huo.
Aitha kauli mbiu ya mkutano huo itasimama kama "Mafao ya fidia haki ya Mfanyakazi na chachu katika kukuza Uchimi wa Viwanda" ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).
Post a Comment