0
DAR ES SALAAM
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewaagiza viongozi wa bodi ya usajili, ubunifu wa majengo na wakadiriaji kuchukua hatua za ikiwemo kuwafutia usajili na kuwachukulia hatua kali wale wote watakapokea au kutoa rushwa katika kupata tenda hama uwajibikaji.

Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa 28 wa wadau wa bodi ya usajili wabunifu wa majengo na wakadiriaji wa wajenzi jijini Dar Es Salaam, amesema ni muhimu kwa bodi kufanya ukaguzi wa kila baada ya muda fulani kwenye miradi ili kuweza kuangalia ubadhilifu unaotoka na vitendo vya rushwa. 

"katika bosi yenu mnapaswa kujitizama na kujipima kupitia utendaji wenu wa kila siku,  ili kujiepusha na rushwa,  maana hapo nyuma mlifahamika kwa kutoa rushwa ili mpate tenda, kitu ambacho kwenye serikali hii ya awamu ya tano hatutaki kusikia" alisema mh. Mbarawa. 

Waziri huyo ambaye amechukua mikoba ya aliyekuwa bosi wake wakati wa awamu ya nne ambaye hivi sasa ni Rais wa JMT John Pombe Magufuri, ameipongeza bodi hiyo kwa kuwakutanisha wataalam wa hapa nchini na wadau wenzao kutoka nchini Kenya, uganda ili wazidi kubadilishana ujuzi na uzoefu sababu teknolojia inakua kwa kasi na kubadirika kila siku. 

Aidha Prof. Mbarawa amewataka wataalu hao kutoa ujuzi kwa vijana wadogo wanachipukia katika fani hiyo ili waweze kupata uzoefu na kuwaandaa kwa ajili ya kuwa wataalam wa siku za usoni, "wakurugenzi na watendaji wa masuala yanayohusu ujenzi hakikisheni vijana wanapewa fursa na kuwekwa kwenye sehemu za miradi mikubwa  ili waweze kujifunza."  alisema waziri Mbarawa. 

Wakati huohuo Mkurugenzi wa bodi ya usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi Albet Munuo amesema, semina hiyo ni sehemu ya muendelezo wa mpango na mafunzo yatakayokuwa yatakayoendelea ambayo bodi imekuwa ikiandaa kwa lengo la  kuwaunganisha wabunifu wa wakadiriaji, wabunifu, wajenzi na wataalam wenye fani hizo za sekta ya ujenzi kukiwa na lengo la kujifunza vitu vipya katika fani hiyo.

Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika ukumbi wa Mlimani city unaendelea huku wadau wa sekta za ujenzi na makampuni ya vifaa vya ujenzi wakiwemo Tanga Cement unategemewa kumalizika siku ya ijumaa kwa wataalam hao kuondoka na mawazo mapya.

Post a Comment

 
Top