LIBERIA.
![]() |
| PHOTO: george Weah akipiga kura. |
Wakati kura zikiendelea kuhesabiwa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi nchini Liberia, mpaka muda huu mwanasoka nyota wa zamani George Opong Weah anaongoza kwa kura zilizohesabiwa mpaka sasa hii ni kutokana na matokeo ya awali yanayoendelea kutoka katika uchaguzi mkuubwa nchi hiyo.
Mgombea anayefuatia kwa karibu ni makamu wa rais Joseph Boakai, ambaye anaongoza katika jimbo moja na mengine yanayosalia ameshika nafasi ya pili.
Atakayetangazwa mshindi anachukua nafasi ya mwanamama wa kwanza Afrika kuwa rais Bi. Ellen Johnson Sirleaf.
Ellen Johnson Sirleaf, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel, anamaliza kipindi chake kwa mjibu wa katiba ya Liberia.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzio NEC zinaonyesha Weah yupo mbele kwa majimbo 11 kati ya majimbo 15 japo zoezi la kuhesabu kura linaendelea.
Mshindi katika uchaguzi huo anatakiwa kupata 50 % ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi, na kama hakuna mgombea atakayefikisha kiwango hicho, uchaguzi wa marudio utapewa nafasi kwa muda usiozidi siku 20 yaani mnamo mwezi Novemba.
Hata hivyo duru mbili ndio zitaamua ushindi wa rais mpya wa nchi hiyo. Uchaguzi huu ni wa kihistoria ambao itakua mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe utawala unakabidhiwa kwa njia ya kidemokrasia kutoka kwa rais anayemaliza muda wake akimkabidhi rais aliyechaguliwa.
![]() |
| PHOTO: kutoka mitandao mbalimbali... |
Miongoni mwa wagombea katika uchaguzi huo ni Joseph Nyumah Boakai, Charles Brumskine, Alexander Cummings, Benoni Urey na George Weah.
Source: BBC


Post a Comment