0
DAR ES SALAAM. 
Sheria inajongea kusimama kila eneo ambalo hapo awali lilikuwa bado halijapewa hama kuonekana halina nafasi kuweza kufuatiliwa kwa karibu hama kufanya uharifu. 

Kufuatia hatua hiyo,  viongozi wote wa makundi ya What's App nchini watatakiwa kutoa taarifa pindi kunapotokea uhalifu utakaofanyika kwenye makundi yao.
Kufanya hivyo kutawasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya mhusika aliyefanya uhalifu huo ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu mtandaoni.

Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi makosa ya kimtandao yameendelea kuongezeka kwa kasi kubwa huku makundi ya What's App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.

Viongozi wa makundi hayo wametakiwa kutowavumilia wahalifu hao na mara moja wametakiwa watoe taarifa polisi.

"Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe utahusika," Amesema Mwangasa.

Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.

Kwa upande wa Viongozi wa dini nao wana nafasi kuwahubilia waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.

"Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa maendeleo," amesema.

Kwa upande wa mamlaka usimamizi wa mawasiliano nchini tcra nayo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano mtandaoni.

Kwa sasa simu za mkononi kwa sasa zimekuwa kama silaha hivyo matumizi yake yanapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top