0
Mara kadhaa kumekuwepo kwa habari za kuzaliwa kwa watoto wawili walioungana na ambao kwa nyakati tofauti wengine wameishi hivyo na wengine kufanyiwa upasuaji ambao kati ya upasuaji kadhaa zinazofanikiwa ni kadhaa.
DRC.
Mapacha waliokuwa wamezaliwa wakiwa wameshikana katika kijiji cha mbali nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, wameponea chupuchupu kwenye safari ya saa 15 kwa njia ya piki piki wakipelekekwa kutenganishwa.

Hata baadaye kusafirishwa kwa njia ya ndege hadi mji mkuu Kinshasa, ambapo walifanyiwa upasuaji na jopo la madaktari wa kujitolea, kwa jumla watoto hao wa wiki moja, wakiwa mikononi mwa wazazi wao walifanya safari ya kilomita 1,400 kwenye barabara mbovu na kwa njia ya ndege.

Watoto hao kwa majina Anick na Destin, watarudishwa kijijini kwao baada ya majuma matatu, na walizaliwa baada ya uja uzito uliochukua wiki 37 mwezi Agosti.

Inakadiliwa kuwa mmoja kati ya watoto wapatao 200,000 huzaliwa wakiwa wameshikana, na kuishi kwao huwa ni finyu hasa sehemu za mbali ambapo hakuna huduma za kiafya, lakini mapacha hawa walizaliwa kawaida tu katika kijiji cha Muzombo magharibi mwa DRC.

Wazazi wao Claudine Mukhena na Zaiko Munzadi walipogundua kuwa watoto wao wanahitaji kufanyiwa upasuaji, waliwafunga blanketi na kuanza safari kupitia msituni kwenda hospitali iliyokuwa karibu.

Kutokana na ukosefu wa vifaa na ujuzi wa kufanya upasuaji huo katika hospitali ndogo, madakaktari waliwahamisha kwenda mjini Kinshasa karibu umbali wa maili 480.

Kufika mjini Kinshasa familia hiyo ilisafirishwaa na ndege ya shirika la MAF, shirika linalotoa huduma za kibinadamu.

"Wako salama, wanalala vizuri na kula vizuri kwa jumla, wako salama, watakuwa hapa kwa wiki tatu zaidi kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa" Dr Junior Mudji alisema.

Dr Mudji anaamini upasuaji huo nduo wa kwanza wa kuwatenganisha mapacha walioshikana nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.



Source: BBC

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top