0

Mitandao ya wahalifu wanaosafirisha pembe za faru kutoka barani Afrika, kila mara wanabadilisha pembe hizo kuwa vito ili kukwepa kutambuliwa katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani.
Shirika la kufuatilia biashara inayohusu wamyamapori imefuchua kuwa pembe hizo hutengenezwa malighafi mbalimbali na kuwa bangili, mikufu na hata kusagwa na kuwa unga.
Kiongozi mkuu wa uchunguzi huo amesema kuwa kwa sasa bishara ya pembe za faru imegeuzwa na kuwa biashara ya vitu vya stahere na inasemekana takriban faru 7,100 wanakadiliwa kuuawa barani Afrika tangu mwaka 2007.
Mpaka kufikia unaposoma taarifa hii karibu faru 25,000 ndio waliosalia, kwenye mbuga kadhaa barani Afrika.

PHOTO: Aina ya vito vitokanavyo na pembe ya faru. 

"Ni jambo la kusikitisha, kwa sababu ikiwa mtu atatembea akipitia uwanja wa ndege akiwa amevaa mkufu ulitengenezwa kutoka kwa pembe ya faru, ni nani atamzuia?”
 alisema Julian Ridemeyer.

Masoko ya pembe za faru yanabaki kuwa yale yale, soko kubwa zaidi likiwa ni China na Vietnam ambapo katika nchi hii kumiliki pembe ya faru hasa kwa watu matajiri kitu cha heshima kubwa.

Source: BBC

Post a Comment

 
Top