0
GEITA.
Mamia ya wananchi, viongozi wa CCM na matajiri wakubwa wa mji wa Geita wamemiminika katika viunga vya mahakama ya hakimu mkazi Geita wakisubiri kupandishwa mahakamani kwa Mbunge wa Geita Vijijini, Joesph Msukuma na madiwani kumi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa kusababisha vurugu zilizotokea Septemba 14 mwaka huu.
PHOTO: Mbunge wa Geita Vijijini Msukuma. 
Walianza kufika mahakamani majira ya saa nane mchana wa leo Jumatatu baada ya taarifa kuanza kuenea kuwa watapandishwa mahakamani lakini hadi kufika majira ya saa 9:20 alasiri Katibu wa CCM Mkoa wa Geita, Adam Ngalawa akatangaza kuwa viongozi hao hawatafikishwa tena mahakamani kutokana na muda wa Mahakama kumalizika.
“Tulikua tunawasubiri wenzetu tuwawekee dhamana lakini nimepigiwa simu sasa hivi kuwa hawataletwa tena mahakamani kwa kuwa muda wa Mahakama umekwisha na taarifa nilizopokea  tumeambiwa wataletwa kesho,” amesema Ngalawa.
Wakizungumza baada ya kauli ya katibu kuwa viongozi hawataletwa mahakamani baadhi ya wafuasi Ikorongo Otto na Masanja Malembeka wamesema kwa sasa hofu imetanda kwa wananchi kwa kuwa huo haukuwa utamaduni uliozoeleka wa kuona viongozi wanakamatwa wakiwa wanadai mali zao.
Awali akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wote wanaoshikiliwa bado wako ndani na watafikishwa mahakamanil leo hata kama muda wa mahakama utakuwa umekwisha watamuomba hakimu.
Amesema dhamana za watuhumiwa ziko wazi kwa kua ni haki ya mtuhumiwa lakini akasema dhamana hiyo inategemea na mazingira ya tukio.
Kamanda amesema bado zoezi la kuwakamata madiwani waliokimbia linaendelea na kuwakata wasiwe wakimbizi badala yake warudi kwenye familia zao kwa kuwa kosa la jinai halina mwisho na lazima watakamatwa kwa uvunjifu wa sheria.
CHANZO:
PHOTO: Walipokuwa wamefunga barabara. 
Mbunge Msukuma na madiwani wa wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia kwenye mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12 milion zinazotokana na kodi ya huduma.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo amethibitishwa kukamatwa kwa Msukuma na kusema askari walimkamata katika eneo la CCM mjini Geita.



Source: Mwananchi.

Post a Comment

 
Top