0
DAR ES SALAAM.
PHOTO: Mwenyekiti wa cha walemavu wa mtindio
wa ubongo Hilal Said akiongea na wanahabari
(hawapo pichani) 
kuhusu athali wanazokumbana nazo wanachama wao.
Chama cha walemavu wa mtindio wa ubongo nchini kimetoa wito kwa serikali kutoa fulsa sawa kwa watu wa kada hiyo ili kuweza kuweka usawa na kuepusha lawama za mara kwa mara zinazotolewa na kada hiyo, ambayo imeonekana kutoweza kufanya kazi yoyote ya uzalishaji.

Akiongea na wanahabari leo jijini Dar Es Salaam mwenyekiti wa chama hicho Hilal Said amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa chanamoto kwa walemuvu hao hapa nchini kutoweza kufanya kazi zote bado nafasi ya kuwaamini ipo na kwa kadiri wanavyoweza kujituma katika maisha yao ya kila siku.

Ameongeza kuwa wao kama walemav wanayo haki kama watu wa kada nyingine na uwezo wao kufanya kazi za kila aina upo ili mradi miundo mbinu iwepo ya kutosha, “mara nyingi watoto wenye mtindio wa ubongo wanantengwa na jamii hata ikifikia mzazi mmoja akifariki akibaki mama kupata mwenzi inakuwa vigumu” amesema Mawanahamisi Hussein.

Ugonjwa wa mtindio wa ubongo ni athali inayotokea kwenye ubongo ambao wa kuendelea, mara kadhaa uonekana katika misuli ambayo usababisha ulemavu na mara nyingi athari hii ujitokeza zaidi kadiri mtoto anavyokuwa.

PHOTO: Kutoka kushoto ni Jane Kumu Mtunza hazima wa chama, katikati Hilal Said mwenyekiti na kulia ni Mwanahamisi Hussein katibu wa chama

Naye katibu wa chama hicho Mwanahamisi Hussein amesema, pamoja na kuwepo kwa unyanyapaa kwa watu hao bado kumekuwepo kwa baadhi ya jamii hasa wanaume kutooa mwanamke ambaye katika jamii yake au mtoto wake anaugonjwa huo.


“unyanyasaji wa jamii hasa kwa sisi wanawake ambao tumeondokewa na mume na kubaki na mtoto mwenye ugonjwa huu bado ni mkubwa kutokana na wanaume wengi kuona mzigo endapo atahamu kuoa mwanamke mwenye mtoto aliye na ugonjwa wa mtindio wa ubongo” amesema Mwanahamisi. 

Post a Comment

 
Top