UGANDA.
Ajali ya Gari T 540 DLC lilipata ajali karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka kuamkia leo tarehe 18/09/2017.
Gari hilo lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikuja kwenye harusi tarehe 16/09/2017 hapa Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es salaam.
Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.
Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.
Naibu Balozi Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona Walio nusurika.
Taarifa hii kwa hisani ya ubalozi wa Tanzania Uganda.

Post a Comment