0
Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kukusanya mapato/kodi kwenye michezo yote ya kubahatisha ikiwa ni sehemu ya majukumu yake iliyokabidhiwa na serikali toka tarehe moja mwezi wa sita mwaka huu kwa mujibu wa sheria ya fedha yam waka 2017.

PHOTO: Mkurugenzi huduma na Elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo
Akiongea na wanahabari mapema leo jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo amesema kitu kigeni ambacho kinaonekana kwa sasa ni kukusanywa na TRA wakapo hapo awali kodi hiyo ilikuwa inakusanywa na bodi ya michezo ya kubahatisha.

“kilichobadirika ni wapi inakusanywa ila viwango ni vilevile” alisema Kayombo.

Kutokana na hilo mamlaka ya mapato nchini inakusanya kodi katika michezo yote ya kubahatisha kama Casino, Sport betting, Slot machines, Lottery na zile za ujumbe mfupi wa maneno (sms).

Kufuatia hali hiyo mchezaji yeyote anayeshinda bahati nasibu katika hizo hana budi kukatwa kodi asilimia 18 na mchezeshaji ambayo huingia serikali moja kwa moja.

PHOTO: kulia,  Afisa mwandamizi Uhusiano kwa umma Rachel na kushoto ni R. Kayombo. 


Kwa upande wa wachezeshaji wao wanatakiwa kuwasilisha asilimia ya mapato yao kwa viwango vifuatavyo, National Lottery 10%, Slot machines shs 32,000/- kwa kila mwezi, Sporsts betting 6%, Casino 15% na sms lottery 30%.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha ukusanyaji wa kodi katika michezo ya kubahatisha ayari TRA kwa kushirikiana na Bodi ya michezo ya kubahatisha imetoa na inaendelea kutoa ufafanuzi kwa waendeshaji wa michezo hiyo hapa nchini sambamba na kutoa elimu.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top