ARUSHA.
PHOTO: Waziri nchi katika Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
George Simbachawene.
|
Waziri
wa nchi katika ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Goerge
Simbachawene amefungua maonesho ya Wakulima na Wafugaji na Uvuvi kanda ya
kaskazini huku akionya viongozi wa ngazi za wilaya kujiondoa katika nafsi zao
endapo wataendelea na utaratibu wa kukusanya mapato katika bidhaa za mazao
zilizoondolewa kodi.
PHOTO: Waziri George Simbachawene akipata
maelezo kutoka
kwa mkulima wa mazao
jamii ya mbogamboga kabla ya
kufungua maonesho ya
kanda ya kaskazini.
|
PHOTO: Waziri George Simbachawene akipata
maelezo kutoka
kwa mkulima wa mazao
jamii ya mahingi kabla ya
kufungua maonesho ya
kanda ya kaskazini.
|
PHOTO: Waziri George Simbachawene (kushoto) akipata
maelezo kutoka kwa mtengenezaji wa viatu vya ngozi.
|
PHOTO: Waziri George Simbachawene akipata
maelezo kutoka
kwa mfugaji wa wanyama jamii ya Ngamia wakati wa kukagua baadhi ya mabanda.
|
PHOTO: Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiongea wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo jijini Arusha. |
ARUSHA.
Waziri
wa nchi katika ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Goerge
Simbachawene amefungua maonesho ya Wakulima na Wafugaji na Uvuvi kanda ya
kaskazini huku akionya viongozi wa ngazi za wilaya kujiondoa katika nafsi zao
endapo wataendelea na utaratibu wa kukusanya mapato katika bidhaa za mazao
zilizoondolewa kodi.
Akizungumza katika
sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo yaliyopo katika eneo la Themi jijini
Arusha ambapo baadhi ya wakulima wanakabiliwa na mavuno hafifu kutokana na
mabadariko ya tabia nchi yaliyopelekea kukosekana kwa mvua za kutosha, Waziri
Simbachawene amewataka wadau wa sekta hizo kujikita katika ukulima wa kisasa wa
mazao yanayovumilia ukame na kutoa matunda kwa muda mfupi.
Pia amewataka
wazalishaji wa bidhaa za kilimo kuboresha vifungashio ili viweze kuwa na
muonekana mzuri pamoja na kukamata soko kutokana na bidha bora
wanazozalisha,pamoja na hilo amewataka wasimamizi wa wazalishaji hao kama SIDO
na TBS kuondoa vipingamizi vinavyoweza kuwafanya wazalishaji wadogo kushindwa kuingia katika ushindani
kutokana na sheria hama mrorongo mrefu.
Hata hivyo amegusia
sheria mpya kwa serikali za mitaa zinazopaswa kufuatwa ili wananchi na viongozi
waweze kuzifuata na kufukia malengo wanayojipangia. Hii hapa taarifa kwa
undani kutoka katika HABARI VIDEO…
Post a Comment