0
ZANZIBAR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi  kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.

PHOTO: makamu wa Rais Samia Suruhu akiongea na wananchi. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati  wa Sherehe ya  Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.

PHOTO: Wananchi wakiwa ufukweni Kuazimisha sherehe ya kizimkazi. 

Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.

Post a Comment

 
Top