PHOTO:
Gari aina ya coaster ambayo iliburuzwa
kwa umbali wa mita 30 kabla ya kusimama hivyo kusababisha vifo na majeruhi.
|
PHOTO: Treni iliyoburuza gari aina ya coaster mara baaada ya kusimama kutoka umbali wa mita 30.
|
MOROGORO:
WANAFUNZI
watatu wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya
basi la abiria aina ya Coaster lililobeba wanafunzi na raia kugonga treni
katika eneo la TANESCO, Morogoro Mjini.
Taarifa za awali
zimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri ambapo Coaster lilikuwa
limebeba wanafunzi wengi wa Shule ya Sekondari ya Kayenzi waliokuwa wakienda
shuleni pamoja na raia wachache lilipokatiza kwenye njia ya treni na kuligonga.
Ikiwa imepita takribani
miezi mitatu tangu wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya Mkoani Arusha wapate
ajali na watu 35 kupoteza maisha, leo majira ya saa moja asubuhi, treni ya
abiria iliyokuwa ikitokea Bara imegongwa na basi la abiria aina ya Coaster lenye
namba za usajili T 438 ABR katika eneo la TANESCO, mjini Morogoro.
Coaster hiyo inayofanya
safari zake kati ya Morogoro mjini na Kihonda ilikuwa imebeba wanafunzi wa
shule tofauti wakielekea shuleni, mmoja wao anadaiwa kupoteza maisha huku wengi
wao wakijeruhiwa kutokana na ajali hiyo tofauti na taarifa zilizosambaa mwanzo
kuwa watu watatu walikuwa wamefariki.
Baada ya kuwatoa
majeruhi na maiti, polisi kwa kushirikiana na wananchi walilisukuma daladala
hilo hadi bondeni na kuipisha treni kuendelea na safari yake.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini humo, Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro, Dkt. Frank Jacob amesema leo asubuhi amepokea maiti ya mwanafunzi
mmoja na majeruhi kadhaa ambapo wawili kati yao hali zao ni mbaya.
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo mwandishi wetu alifika haraka eneo la tukio na kukuta umati mkubwa wakimshushia kichapo dereva wa daladala hiyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakati akitaka kukimbia baada ya tukio hilo.
Baada ya kutokea kwa ajali hiyo mwandishi wetu alifika haraka eneo la tukio na kukuta umati mkubwa wakimshushia kichapo dereva wa daladala hiyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja wakati akitaka kukimbia baada ya tukio hilo.
Post a Comment