PHOTO: Uongozi wa shule ya Usa River Academy. |
ARUSHA.
Wanafunzi wa darasa la
saba na wale wa kidato cha nne nchini wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu
masomo yao kuanzia mwenzi wa 9 na 10 ikiwa ni hatua nyingine ya kutoka hatua
moja ya elimu kwenda hatua nyingine ya elimu kwa madara ya juu kutoka pale
walipo.
Katika hotuba ya sherehe
ya mahafari ya 14 ambayo imefanyika katika shule ya msingi na sekondari ya Usa
River Academy iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha, Mkuu wa shule hiyo madam
Eva Ngowi amesema dunia ikiwa katika zama za sayansi na kukiwa na ushindani mkubwa
wa elimu ambayo haiwezi kuwa na manufaa kwa wananchi wanchi husika endapo
haitatumika ipasavyo.
Katika risala yao kwa
walimu, wazazi na wageni waliofika shuleni hapo wanafunzi wanaohitimu masomo
wakiwemo wa darasa la saba na kidato cha nne wameelezea matumaini yao kutokana
na uongozi wa shule na walimu kujitoa kuwafundisha masomo na maisha ya kujitegemea
wanasema “Maisha
ni sehemu yenye mfululizo wa matukio yawe mema hama mabaya bila kujali jinsi
ambavyo unaweza kuthibiti hali inayoweza kujitokeza…”
NDANI YA HABARI: undani wa habari hii utaipata kupitia ukurasa wetu wa habari katika video uliopo kulia kwa ukurasa
huu unaosoma....
Post a Comment